Baada ya miezi ya maneno, kejeli na hadi kuzomewa hatimaye Rais Mstaafu Bw. Benjamin Mkapa amezungumza wiki iliyopita akikanusha madai kuwa ametajirika visivyo halali. Zaidi ya yote amedai kuwa yeye anaishi kwa pensheni yake kama anavyoishi Mzee Mwinyi na yakuwa wanaozua maneno ya yeye kuwa "fisadi" ni watu ambao kwa maneno yake walitaka "awapendelee" alipokuwa madarakani na yeye "hakuwapendelea".
Na kabla wingu la utetezi wake huo halijatua kampuni ya Makaa ya Mawe ya Kiwira imejitokeza baada ya miezi kuhusishwwa na Urais wa Mkapa na kutangaza kuwa Rais Mkapa si mmiliki wa mgodi huo na hivyo kujaribu kuzima madai hayo. Hata hivyo mambo yafuatayo ni ya kuangalia na tuone kama utetezi wa Mkapa mwenyewe na Kiwira unatosha kumsafisha Rais Mstaafu.
Unaweza kusoma mjadala huu kwenye Jamiiforums.com mada ya "Kiwira yamsafisha Mkapa"
Tanpower Resources ilisajiliwa 29/12/2004 na kupewa namba 51080 ikiwa na dhumuni kuu la kwanza kuchimba mkaa wa mawe nakuzalisha umeme, wakati huo Mkapa bado ana hisa na alijua sababu za kuanzishwa kwake. Wakati inasajiliwa wanahisa walikua ANBEM hisa 200,000 na aliyesaini ni Anna Mkapa, Devconsult ya Yona na Mwanae (hisa 200,000), Universal Tech (hisa 200,000), Choice Industries ya Mbuna (200,000) na Fosnik Enterprises ya Nicholus Mkapa na mkewe Foster wakiwa wameiga jina la kampuni ya baba na mama zao ya ANBEM (wao wakiwa na hisa 200,000) na aliyesaini ni Nico
-----Lakini jambo la hatari ni kwamba, kabla hata ya TANPOWER kusajiliwa ilikwishaanza kufanya kazi na Evans Mapundi akiwa Mkurugenzi wake, alifanya mawasiliano Desemba 15 na wakatembelea Kiwira Desemba 18 na 20, kwa baraka za Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona. Yona akiwa pia mmoja wa wanahisa wa kampuni hiyo.
----Mkapa na Mkewe kupitia ANBEM walijitoa TANPOWER Februari 21, 2005 ikiwa tayari hata mkataba wa ubia kati ya TANPOWER na Kiwira umekwishaandaliwa na Yona akiwa Waziri wa Nishati na Madini.... Hata baada ya Kujitoa, Mwanae Nico na mkewe Foster na baba mkwe wao Mbuna walikua ndani ya Kiwira.
----Ni mwaka huo ambao Yona na bosi wake waliitosa STAMICO na kuchukua eneo jingine lenye hazina kubwa ya mkaa wa mawe liitwalo Kabulo rig ambalo serikali ilikopeshwa USD milioni 50 kufanya utafiti. STAMICO hadi sasa wanalilia eneo hilo ambalo limechukuliwa na TANPOWER/Kiwira bure
http://www.jamiiforums.com/photos/Mkapa1.jpg
http://www.jamiiforums.com/photos/Mkapa2.jpg
SWALI
Je Umeridhika na utetezi na jitihada za kujisafisha za Rais Mkapa. Waandishi waache kumsakama Rais mstaafu kwa sababu Kiwira wamesema hahusiki nayo?